Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Matembezi hayo yalifanyika katika mazingira ya utulivu na nidhamu, huku yakihusisha waumini wa rika mbalimbali waliovalia mavazi ya maombolezo na kubeba mabango yenye ujumbe wa amani, haki na kupinga dhuluma. Washiriki walisisitiza kuwa ujumbe wa Ashura unaendelea kuhamasisha jamii kusimamia ukweli, uadilifu na heshima ya utu wa binadamu.
Katika nasaha zilizotolewa, viongozi wa dini walieleza kuwa mapambano ya Imam Hussein (as) yalikuwa ni kwa ajili ya kulinda misingi ya Uislamu na maadili ya kibinadamu, hivyo ni wajibu wa waumini kuendelea kuenzi na kuishi kwa kuzingatia mafundisho hayo.
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |










Maoni yako